Friday 15 April 2016

Kigogo Aikacha Chadema Amfuata Magufuli CCM

Kigogo Aikacha Chadema Amfuata Magufuli CCM

Tarehe April 15, 2016
Chadema
Chadema
Kigogo wa Chama cha Demokrsaia  na Maendeleo (Chadema) ambaye alikuwa  Mwenyekiti wa chama mkoa wa Mwanza   Andrian Tizeba ametangaza kuhamia Chama  cha Mapinduzi (CCM).
Aidha, Bw.Adrian  leo amejiunga rasmi na CCM wilayani  Sengerema tawi la Lugata  ambapo  alitangaza kujivua uanachama wa chadema Machi 29 mwaka huu baada ya kusimamishwa uongozi kwa muda wa mwaka mmoja, na kutangaza kuachana na siasa, amekabidhiwa kadi hiyo  na katibu wa tawi hilo Alfred Mwambala.
Kwa upande wake Tizeba amesema uamuzi wake si wa kulazimishwa na mtu bali, ameona ni vema arudi kwenye chama chake cha awali   kutokana na kuridhishwa na  utendaji wa Rais Dkt.  John Magufuli.

clouds stream