Friday 15 April 2016

Mradi Wa DART Sasa Kuanza Mei 10

Mradi Wa DART Sasa Kuanza Mei 10

Tarehe April 15, 2016
10262227_717689465039977_2529648417247638500_n
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, TAMISEMI, George Simbachawene amesema mradi wa mabasi yaendayo kasi (DART) utaanza rasmi Mei 10, mwaka huu wakati akifanya majumuisho ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa.
Simbachawene amesema kuwa wadau wa mradi huo wamemhakikishia kuwa mabasi hayo yataanza kutoa huduma ya usafiri ifikapo Mei 10 baada ya kukutana nao na kuzungumza kwa kirefu.
“Tumeambiwa kuwa mradi huu una mikataba mingi na kwamba bado kuna majadiliano makubwa ya mikataba hivyo hatuwezi kulazimisha maana unaweza kujikuta ukitengeneza mikataba mibaya na tunaendelea na mijadala ya mikataba hiyo ingawa uwazi ni muhimu sana,” amesema.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawalana Serikali za Mitaa, Jasson Rweikiza amesema kamati yake imeshatembelea mradi huo zaidi ya mara nne na kugundua tatizo linalokwamisha ni fedha na kuitaka Serikali kuhakikisha inatoa fedha ili huo uanze mara moja kama ilivyokusudiwa.
Amesema ni muhimu sana kwa mradi huo kukamilika na kuanza kutoa huduma maramoja ili kupunguza kero ya usafiri kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wanaoteseka na tatizo la usafiri na foleni za barabarani.

clouds stream