Friday 22 April 2016

Daladala Zatakiwa Kupotea Katikati Ya Jiji Ifikapo Mei 2

Daladala Zatakiwa Kupotea Katikati Ya Jiji Ifikapo Mei 2

Tarehe April 21, 2016
Daladala zote zinazofanya safari zake katika maeneo ya katikati ya Jiji la Dar es Salaam zimetakiwa kuwa zimeondoka iikapo Mei 2, mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa na Msemaji wa Mradi wa Mabasi yaendayo Kasi (DART), Sabri Mabrouk ambaye amedai ya kuwa tayari wamiliki wote wa mabasi hayo wamekwishalipwa fidia ili wabadili njia zao za usafiri nje ya katikati ya Jiji.
“Wamiliki wote wa mabasi wamekwishalipwa fedha zao tangu Desemba mwaka jana na sasa hakuna yeyote anayedai hivyo wana siku saba tu kuhakikisha kuwa wamekwishaondoka katika barabara hizo kabla ya Mei 10,” amesema Mabrouk ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Mkoa wa Dar es Salaam (DARCOBOA).
Tayari mabasi yaendayo kasi yamekwishaanza majaribio ya kupita katika njia zake huku huduma hizo zikitarajiwa kuanza rasmi Mei 10, mwaka huu.

clouds stream