Saturday 9 April 2016

Ridhiwani Kikwete Aibuka, Aikana ‘Kweupe’ Kampuni Ya Lugumi

Ridhiwani Kikwete Aibuka, Aikana ‘Kweupe’ Kampuni Ya Lugumi

Tarehe April 9, 20161
1
Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete
Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete, amekanusha taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii kuwa yeye ni mmoja wa wamiliki wa kampuni ya Lugumi, inayodaiwa kupewa zabuni ya kufunga mashine za kuchukua alama za vidole kwenye vituo vya Polisi.
Ridhiwani ambaye ni mtoto wa Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete amesema yeye hahusiki na kampuni yoyote ya Lugumi ingawa wana urafiki wa kawaida na mmiliki wa kampuni hiyo, Said Lugumi.
“Hapa ni watu tu wanaamua kuingiza tu maneno yao, haya maghorofa ninayotajwa kumiliki Dar es Salaam hata sijawahi kutembelea ujenzi wake, wameamua kuniingiza, Lugumi nafahamiana naye binafsi tu lakini wananiingiza,” alisema Ridhiwani
Hivi karibuni Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ilitoa siku saba kwa Jeshi la Polisi nchini kupeleka mkataba walioingia baina yao na Kampuni ya Lugumi baada ya kampuni hiyo kufunga mashine za kuchukua alama za vidole kwenye vituo 18 vya polisi badala ya 108 kama ilivyoainishwa kwenye mkataba.
Kwa mujibu wa PAC, mkataba huo ulikuwa wa Sh bilioni 37 pamoja na kodi na kwamba hadi sasa kampuni hiyo imeshapewa asilimia 99 ya fedha zote lakini imeshindwa kumaliza kazi iliyopewa.

clouds stream