Friday 29 April 2016

EPL Leo Arsenal Dimbani Na Norwich City

EPL Leo Arsenal Dimbani Na Norwich City

Tarehe April 29, 2016
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger akiwa na mshambuliaji wake Olivier Gioud
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger akiwa na mshambuliaji wake Olivier Gioud
Ligi kuu ya soka ya England inaendelea tena hapo kesho kwa michezo kadhaa,Everton ni wenyeji wa Bournemouth, Newcastle United wanawaalika Cristal Palace,Stoke city dhidi ya,Sunderland,Watford watachuana na Aston Via,West Brom wanawaalika West Ham United, na Arsenal watakuwa wenyeji wa Norwich city.
Hadi sasa ligi hiyo inaongozwa na Leicester city yenye alama 76,Tottenham alama 69,Man city alama 64 sawa na Arsena yenye alama 64.
Katika nafasi ya mwisho katika msimamo Timu za Aston via na Newcastle ndio Timu zinazoburuza mkia kufuatia kuwa na alama chache kuliko Timu zote,Idhaa ya Kiswahili ya BBC itakutangazia mechi kati ya New castle Unite na Cristal palace.

clouds stream