Wednesday 6 April 2016

Mhadhiri UDSM Ateketea Kwa Moto Kwenye Gari Lake




Mhadhiri UDSM Ateketea Kwa Moto Kwenye Gari Lake


Tarehe April 6, 20161 (1)
1 (1)

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Idara ya Sayansi na Uhandisi wa Kompyuta (CoICT), Dk Richard Mgaya amefariki baada ya kuteketea ndani ya gari lake jijini Dar es Salaam juzi.
Gari la Dk Mgaya liliteketea baada ya kugongana na lori katika eneo la Mbezi Africana, Wilaya ya Kinondoni usiku wa kuamkia juzi na kuwaka moto uliosababisha kifo chake.
Kabla ya kutambulika, picha mbalimbali zilisambaa katika mitandao ya kijamii zikionesha gari aina ya Toyota Prado likiwa limeteketea na baadaye ilibainika kuwa aliyekuwa katika gari hilo ni Dk Mgaya.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Christopher Fuime alisema gari la Dk Mgaya liliteketea na hata kushindwa kujulikana dereva wa gari hilo lakini baadaye ndugu wa marehemu walithibitisha kuwa gari hilo lililoteketea na dereva aliyekuwemo ni Dk Mgaya.
“Lile gari liliungua na hakuna kitu kilichopatikana, hata wakati polisi wanafika eneo la tukio walikuta tayari dereva amekuwa majivu kutokana na kuteketea kwa moto… labda baada ya kupima vinasaba ndio itathibitika kama ilikuwa ni yeye,” alisema Kamanda Fuime.

clouds stream