Tuesday 14 March 2017

Maharamia wanadai fedha kuachia Meli, Somalia

Meli katika pwani ya Somalia

Meli katika pwani ya Somalia
img-20161130-wa0008

Kikosi cha Jeshi la majini la kupambana na Uharamia la Umoja wa Ulaya, kimethibitisha kuwa watu wenye silaha wanataka kupewa fedha, kuiachia meli ya mafuta iliyokamatwa nje kidogo ya pwani ya Somalia siku ya Jumatatu.

Kikosi hicho kimesema kimefanya mawasiliano kwa njia ya simu na mmiliki wa meli hiyo, ambaye amesema meli na wafanyakazi wake walikamatiwa Kaskazini mwa pwani ya Puntland.

ARIS-13 ilikuwa ikisafiri kutoka Djibouti kwenda katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu wakati ilipotuma alama ya hatari ikisema kuwa inafuatwa na boti inayokwenda kasi.

Hii ni mara ya kwanza kwa meli ya kibiashara kutekwa nyara baharini katika eneo la pwani ya Somalia tangu mwaka 2012.

Maharamia walikuwa wamepiga kambi katika maeneo hayo mpaka pale vikosi vya jeshi la majini vya Umoja wa Ulaya vilipoanza kufanya doria na kudhibiti hali hiyo.

clouds stream