Thursday 9 March 2017

Mdogo Wa Gwajima ‘Amlipua’ Kaka Yake Na Kumkingia Kifua Makonda

Methusela Gwajima.
Methusela Gwajima.
img-20161130-wa0008

Mdogo wa Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, Mwanasheria, Methusela Gwajima leo ameibuka na kuvitaka vyombo vya dola kumuonya Askofu Gwajima juu ya tabia yake ya kufatilia tuhuma za watu wengine wakati na yeye pia ni mtuhumiwa.

Amesema mchungaji huyo anatakiwa aache kutumika na kuhoji kuna nani nyuma yake kwani kama mchungaji hawezi kujiingiza kwenye malumbano na mipasho ya kidunia.

Ameendelea kusema kuwa sakata la vyeti vya Makonda linapaswa kuachwa kwa mamlaka husika kuchunguza kwani kumuandama sana inaweza kusababisha watu wengine siku zijazo kuogopa kujihusisha katika vita ya kupambana na madawa ya kulevya.

“Serikali imemlea sana Gwajima na Waziri wa Mambo ya Ndani anatakiwa amuangalie sana kwani ana tuhuma nyingi ikiwemo kudai kuwa angemfufua baba wa watoto yatima ilhali yeye anajua wazi ya kuwa hajawahi kufufua hata panya,” amesema Methusela.

Aidha, ameongeza kuwa tabia ya kubeza shughuli za maendeleo zinazofanywa na serikali sio tabia njema na haiisadii nchi kwani vita ya madawa ya kulevya ni ngumu na hugharimu maisha na kuwataka watanzania wote kuunga mkoni juhudi za kutokomeza madawa ya kulevya hasa katika Jiji la Dar es Salaam.

Amesema anafahamu yeyote atakayejitokeza kuunga mkono juhudi za kupambana na madawa ya kulevya ataandamwa tu na hivyo kwa namna ya pekee anamshukuru Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paulo Makonda kwa juhudi zake na atakumbukwa na vizazi vyote kwa kujitoa mhanga kusimamia vita ya madawa ya kulevya Jijini Dar es Salaam kwani sasa kila mmoja amefahamu athari za madawa ya kulevya hadi kwa watoto wadogo ndio maana anaandamwa kila kona.

Mchungaji Gwajima ni mmoja wa watu waliotajwa na Makonda kama watu wanaojihusisha na biashara na matumizi ya madawa ya kulevya na tangu wakati huo amekuwa akimuandama Makonda katika nyumba yake ya ibada akimtuhumu kutumia vyeti vya mtu mwingine na kumtaka kuweka hadharani vyeti vyake halisi.

clouds stream