Rais wa Palestina Mohamud Abbas

Ikulu ya white house inasema kwamba rais Donald Trump amemwalika kiongozi wa Palestina, Mohamud Abbas, nchini Marekani hivi karibuni.
Bwana Trump amemwalika Abbas baada ya mazungumzo ya kwanza ya simu na kiongozi huyo tangu aingie maamlakani.
Trump amependekeza kuhusika katika juhudi za amani mashariki ya kati, japo viongozi wa Palestina wanalalamika kwamba sera ya kigeni ya rais Trump inaonekana kupendelea Israeli.
Hakujakuwa na mazungumzo ya amani ya haja kati ya Israel na Palestina tangu mazungumzo ya amani yalioanzishwa na Marekani kugonga mwamba mnamo mwezi Aprili 2014.
Msemaji wa Trump Sean Spicer alithibitisha siku ya Ijumaa kwamba rais wa Marekani alimualika Abbas katika ikulu ya Whitehouse hivi karibuni.
