Polisi wanatuhumiwa kutumia nguvu kubwa kukabiliana na waandamanaji

Maelfu ya raia wamekusanyika katika maeneo tofauti nchini Urusi wakiandamana kupinga kile wanachodai matumizi mabaya ya fedha za umma.
Mkusanyiko mkubwa upo katika mji wa Moscow ambapo shinikizo ni kumtaka waziri mkuu wa Urusi Dmitry Medvedev kujiuzulu.
Wanaharakati wanasema kuwa hadi sasa watu 800 wanashikiliwa na Polisi.
Maandamano haya yanatajwa kuwa ni makubwa zaidi ya yale yaliyowahi kutokea nchini Urusi kwa miaka mingi, ambapo wanadai kuwa waziri mkuu wao Dmitry Medvedev amekuwa akutumia fedha za umma
katika mambo yake binafsi kwa kujenga majumba kifahari, kununua boti za kifahari, mashamba ya mvinyo na jumba la kufugia bata.
