Thursday 9 March 2017

Kafulila Aibuka Na Mambo Matano Sakata La Vyeti Feki

Image result
Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila
img-20161130-wa0008

Aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila ameibuka na kuongea mambo matano kuhusiana na sakata la vyeti feki linalomuandamana Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Kafulila amesema yafuatayo;

Kwanza ni ushauri wangu kwamba Makonda amsaidie Rais ama kwa kuonesha vyeti vyake vyote kuondoa utata au ajizulu ili serikali iendelee na mambo mengine. Obama alipotuhumiwa kuhusu uraia wake USA alifanya kazi ndogo tu ya kuweka vyeti vyake vyote hadharani na akawa amefunga utata wa uraia wake. hivyo ni vema Makonda afanye hivyo kama anavyo au akae pembeni kwani nchi ni muhimu kuliko mahusiano yake na Rais.

Rais anapaswa kujua kuwa hoja ya jinai ya kughushi vyeti inayopigiwa kelele inahusu pia umakini wa mamlaka yake kama mteuzi wa Makonda kwamba kuna shida ya vetting. hivyo kuondoa hilo ni kuchukua hatua stahiki. Hakuna namna Rais atamlinda Makonda na akabaki na sifa ya kuwa Rais anaesimamia haki na Usawa. itafanya aonekane kama waliomizwa na ukali wake katika kusimamia sheria nikwasababu hawakuwa na ukaribu nae na zaidi itafanya aonekane Rais wa kawaida sana kwa kulinda uovu kwa sababu za binafsi.Hivyo ukimywa wa Rais unafanya dhamira yake ya uzalendo ihojike kwani sio kawaida yake.

Mamlaka kama Sekretariet ya Maadili ya Uongozi ilipaswa kuwa imeshachukua hatua kuondoa wingu hili kwani kinachojadiliwa hapa mbali zaidi ya jinai pia kinahusu uadilifu wa Kiongozi(intergrity). ukimywa wa taasisi hii ni mfano mbaya wa namna taasisi zinavopigwa ganzi pindi haki inapotakiwa kutendeka lakn inagusa maslahi ya Rais. huu ni uzoefu niliopata kuona hata kwenye sekata la escrow.likitokea jambo ambalo Rais ana maslahi taasisi zetu zimekuwa nzito na kigugumizi kuchukua hatua ipasavyo.

Chuo cha Uvuvi walichomsajili kwa cheti cha form4 ambacho anatuhumiwa kuwa sio chake pamoja na Chuo Kikuu ni taasisi ambazo mjadala huu unahusu heshima ya taasisi hizo. hivyo ilipaswa zijitokeze kuthibitisha au kukanusha. ukimya wao unaashiria hofu yao kwasababu kaguswa mtoto wa mfalme! Huu ni mfano mbaya kabisa kwa taasisi za taaluma kwamba zinaweza kuwa za hovyo kiasi hiki.

Kibaya zaidi ni ukimya wa NECTA ambao ni mamlaka ya kutoa vyeti. sasa cheti kinachosumbua hapa ni cha form4 ambacho ni mali yao. lakn kwa woga wamekaa kimya kuficha ukweli na kuacha mjadala wa cheti uwe kati ya Askofu na RC na watanzania wakati wao ambao ni mamlaka sahh kuondoa utata wamekaa kimya kwa hofu ya kugusa mtoto wa mfalme.. Hili ni fundisho la kwann nchi hii haiendelei kwasababu taasisi hizi haziko imara kutimiza majukumu yake kisheria bali zinafanya majukumu yake kwa kadiri ya mapenzi ya mteule wao.

clouds stream