Balozi wa Korea Kaskazini nchini Malaysia apewa saa 48 kuondoka nchini humo.

Malaysia imemfukuza balozi wa Korea Kaskazini kuhusiana na kifo cha Kim Jong nam ,ndugu wa kambo wa kiongozi wa Korea kaskazini.
Kang Chol amepewa agizo la kuondoka nchini humo katika kipindi cha saa 48, alisema waziri wa maswala ya kigeni nchini humo.
Kim Jong nam ndugu wa kambo wa Kim Jong un ,alifariki wiki tatu baada ya wanawake 2 kumpaka kemikali ya sumu usoni mwake katika uwanja wa kuala Lumpur .
Malaysia haijailaumu Korea kaskazni kwa shambulio hilo lakini kuna shauku kwamba Pyongyang ilihusika.
Balozi wa Korea Kaskazini, Bwana Kang alitangazwa persona non grata{ hatakiwa nchini humo} siku ya Jumamosi baada ya kusema kuwa taifa lake haliweza kuamini uchunguzi uliofanywa na Malaysia na kwamba uchunguzi huo ulikuwa ukiingiliwa.
