Wednesday, 4 February 2015

Jordan yathibitisha Ruban kuuawa na Islamic State

Jordan yathibitisha Ruban kuuawa na Islamic State

Rubani wa Jordan Luten Moaz al-Kasasbeh wakati wa uhai wake.
Rubani wa Jordan Luten Moaz al-Kasasbeh wakati wa uhai wake.
Rubani wa Jordan Luten Moaz al-Kasasbeh wakati aliposhikiliwa na wanamgambo wa Islamic State.
Rubani wa Jordan Luten Moaz al-Kasasbeh wakati aliposhikiliwa na wanamgambo wa Islamic State.
Jordan imethibitisha kifo cha rubani Moaz al-Kasasbeh baada ya picha ya video kuchapishwa katika mtandao na kikundi cha Islamic State, IS kilichodai kumwonyesha akichomwa moto angali hai.
Video hiyo inamwonyesha mtu akiwa amesimama katika kisanduku kilichozingirwa na moto. Mfalme Abdullah wa Jordan, amempongeza Luteni Kasasbeh kama shujaa, akisema Jordan lazima “iungane” katika machungu.
Rubani huyo alikamatwa wakati ndege yake ilipotua karibu na mji wa Raqqa, nchini Syria, wakati wa operesheni ya kijeshi dhidi ya IS mwezi Desemba. Picha hiyo ya video ilitumwa Jumanne na kusambazwa kupitia mtandao wa Twitter unaojulikana kama chanzo cha habari za propaganda za kikundi cha IS.
Video hiyo ya dakika 22 inamwonyesha rubani wa Jordan akipita katika maeneo ya vifusi huku akiwa ameelekezwa mtutu wa bunduki. Vifusi hivyo vimesababishwa na mashambulio ya anga ya majeshi washirika yakiwalenga wapiganaji wa Kiislam.

clouds stream