Wanajeshi Chad waingia Nigeria kupambana na Boko Haram
Juma lililopita, Vikosi vya Chad viliripotiwa kuingia mjini Malumfatori, mji ulio karibu na mpaka kati ya Chad na Niger, baada ya mapambano dhidi ya Wanamgambo.
Kiongozi wa kundi la Boko Haram, Aboubakar Shekau ametishia kuanzisha matawi ya wanamgambo katika maeneo mengine nchini Nigeria, Niger, Chad na Cameroon.
Umoja wa Afrika una mpango wa kuunda kikosi cha Wanajeshi 7,500 kupambana na Boko Haram.