Wanafunzi wajawazito kurudi shuleni baada ya kujifungua
Baada ya Serikali kuitikia wito wa wazazi, wanafunzi na walimu wao kuruhusu wanafunzi wote wajawazito kurudi shule baada ya kujifungua.
Akiongea Sada Fakih kutoka kwenye kamati ya Elimu amesema inabidi kuwapa moyo vijana wetu na sio kuwakatisha tamaa kwa kuonekana hawafai kwenye jamii, pia Bi Sada akaongelea kuhusu chanzo kikubwa cha vijana kujiingiza kwenye mapenzi wakiwa wadogo ni miamko, kutokuwa na elimu kuhusu mapenzi.
Pia Bi Sada aongelea mkutano aliowakutanisha walimu, wazazi na wanafunzi ili kuweza kuwatoa msongo wa mawazo kwa watoto wao wa kike ili kuingia kwenye maisha mapya ya kurudi mashuleni kwao.
Takwimu zinasema kwa mwaka 2012 zinaonyesha takribani wanafunzi wa kike 610 waliacha shule kutokana na mimba huku kwa wanafunzi wa kike kwa sekondari mwaka 2011 takribani wanafunzi 5,157 waliacha shule kikwazo kikiwa ni mimba.