Tuesday 8 November 2016

Waziri Wa Elimu Mstaafu Joseph Mungai Afariki,JPM Amlilia

 Aliyewahi kuwa waziri wa Elimu Tanzania Joseph Mungai enzi ya uhai wake.
V 2
Aliyewahi kuwa waziri wa Elimu Tanzania Joseph Mungai enzi ya uhai wake.

Baada ya kifo cha Spika wa Bunge Mstaafu Mzee Samweli Sitta,Tanzania imepata pigo jingine kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa waziri wa Elimu Tanzania Joseph Mungai.

Kwa mujibu wa Geofrey Mungai mtoto wa Marehemu amesema marehemu alipelekwa hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kuanza kutapika mfululizo na kudhaniwa kwamba alikuwa amekula kitu kibaya.

Mzee Mungai alifikishwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu hadi umauti unamfika.

Kufuatia kifo hicho Rais Dkt.John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi ambapo amesema Mzee Mungai alikuwa mchapakazi, mtu aliyesimamia alichokiamini, mpenda maendeleo aliyefanya kazi kwa ushirikiano.

Mungai enzi ya uhai wake alikuwa Mbunge mstaafu wa Jimbo la Mafinga mkoani Iringa na aliwahi shika nyadhifa mbalimbali serikali ikiwemo Waziri wa Elimu.

Mungu ailazo Roho ya marehemu mahali pema peponi.Amina

clouds stream