Sunday 13 November 2016

UDA Wakanusha Kauli Ya Mdee

uda
V 2
Kampuni ya Simon Group inayomiliki mabasi ya UDA na mradi wa mabasi yaendayo haraka kwa ubia na Serikali imekanusha vikali madai ya Mbunge wa Kawe, Halima Mdee kuwa kampuni hiyo iliuzwa kwake kinyemela.
Msemaji wa SGL, Deus Bugaywa alisema madai hayo siyo ya kweli.
Akichangia hoja hivi karibuni bungeni Dodoma, Mdee alisema kampuni ya UDA haikuuzwa kihalali kwa Simon Group Ltd, Waziri husika hakuridhia kihalali uamuzi wa Baraza la Jiji, hivyo UDART iliuzwa kinyemela na SGL ilitumia rasilimali za UDA kupata mkopo wa kuendesha Udart.

clouds stream