Monday 7 November 2016

Spika Mstaafu Samuel Sitta Afariki Dunia

samuel-sitta
V 2
Marehemu Samuel Sitta.
Spika Mstaafu, Samuel Sitta, 74, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo nchini Ujerumani alipokuwa akipatiwa matibabu.
Kwa mujibu wa mtoto wa marehemu ambaye pia ni Meya wa Kinondoni, Benjamin Sitta, marehemu amekata kauli usiku wa kuamkia leo alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa tezi dume uliokuwa ukimsumbua.
Amesema watatoa taarifa zaidi juu ya msiba huo kadiri watakavyokuwa wanapata taarifa kutoka nchini Ujerumani ambapo mke wa marehemu, Magreth Sitta yupo huko.
Marehemu Sitta alikuwa mmoja wa wanachama wa CCM waliotangaza nia ya kutaka ruhusa ya kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana katika kinyang’anyiro cha Urais.

clouds stream