Thursday 6 March 2014

BURUDANI: LIONEL MESSI AONGELEA KUTAPIKA KWAKE UWANJANI.

Camera kibao na wapiga picha lukuki walifanikiwa kunasa tukio la mchezaji machachari lionel messi akitapika uwanjani mnamo dakika ya saba ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki kati ya Argentina na Romania ulioishia kwenye suluhu ya bila kufungana. Tukio hilo lilizua mjadala juu ya afya ya mchezaji huyo ukizingatia kua kuna mechi muhimu katika ya Barceloba na Real Madrid hivi karibuni. Tukio la messi kutapika lilimkumba tena mwaka 2011 akiwa Barcelona walipocheza na Real madrid na pia katika mechi kati ya Argentina na Bolivia mwezi machi mwaka 2013.
Baada ya mechi, messi iliiambia TyC sports kua hali hio inamtokeaga kila mara. Akazidi kusisitiza kua imeshawai kutokea hata akiwa klabu yake ya sasa na sio kitu cha kushangaza sana kwake.
Kocha wa timu ya Argentina Alejandro Sabella alis
ema tatizo la messi sio kubwa kama watu wanavyodhani. Lilitibiwa na glass ya maji tu hivyo washabiki wasiwe na shaka juu ya afya ya messi

clouds stream