Friday 21 March 2014

WASANII WA HIPHOP WALIO INGIZA PESA NYINGI ZAIDI MWAKA 2013

Kutokana na orodha ya watu waliopata pesa nyingi sana mwaka jana, Forbes imeainisha wasanii wa hiphop duniani walioingiza pesa nyingi zaidi.
list hii ni kama ifuatavyo:

1. DIDDY ($50 MILLION)
Sean Combs amechukua taji hili kwa mara ya kwanza mwaka 2013 akiwa na mapato makubwa kutokana na kinywaji chake cha Ciroc Vodka pamoja na vyanzo vingine kama nguo za sean John, label yake ya mziki ya BadBoy na Cable Channel Revolt.

2. JAY-Z ($ 43 MILLION)
Jay-z ameweza kukusanya pesa nyingi kwa kupitia label yake ya Roc Nation,  live performances kibao za bei ghali, champagne yake ya Armand de Brignac na pia alipata zaidi ya $5 million kutoka samsung kwa ajili ya album yake mpya ya Magna Carta.

3. DR. DRE ($40 MILLION)
Pamoja na kuuza sehemu ya Beats by Dre, Dr.Dre bado anapata pesa nono kutoka kwa sehemu ya kampuni hio aliyobakiza na imemuezasha kua na pesa nyingi sana kwa mwaka 2013. Pia aliweza kuingia ubia na Jimmy Iovine kufanya mchakato wa kucheza nyimbo moja kwa moja toka kwenye internet (streamming) ambayo pia imekuza mapato ya Dre.

4. NICKI MINAJ ($29 MILLION)
Miaka miwili baada ya kua mwanamke wa kwanza wa hiphop kuingia kwenye orodha ya kuingiza pesa nyingi, nicki minaj ameweza kuingiza kiasi cha $29 millon mwaka 2013. Hii imetokana na matamasha, mauzo ya album zake, kuwa judge katika American idol na pia pesa kutoka kwenye matangazo ya pepsi.

5. BIRDMAN ($21 MILLION)
Kiongozi wa cash money ameweza kuendelea kuingiza pesa nyingi sans kutokana na label yake ya mziki na pia mauzo ya Vodka zake pamoja na uwepo wa watu kama lil wayne, nicki minaj na drake katika label yake.

6. KANYE WEST ($20 MILLION)
Kanye west ameweza kuingiza kiasi hiki cha pesa mwaka jana kwa sababu kuu ya album yake ya Yeezus ambayo ilimuweka kwenye chati na kumfanya awe mmoja kati ya wana hiphop wanaitwa zaidi kwenye shows.

7. LIL WAYNE ($16 MILLION)
Pamoja na kufanya  show chache sababu ya ugonjwa, lil wayne amefanikiwa kuingiza pesa hio sababu ya mauzo ya album yake ya Iam Not A Human Being II. Pia mauzo ya mavazi yamechangia mapato ya rapa huyu kwa mwaka jana.

8. WIZ KHALIFA ($14MILLION)
Akiwa amefanya zaidi ya shows 75 wiz khalifa kaingiza pesa nyingi akiwa na mauzo mazuri katika album yake ya Rolling Papers.

9. LUDACRIS ($12 MILLION)
Pamoja na mauzo ya album ya ludacris Ludaversal kutofanya poa sana, ludacris amefanikiwa kutengeneza pesa nzuri kwa sababu ya mauzo ya headphones zake za Soul by Ludacris, kinywaji cha Conjure Cognac pamoja na filamu ya Fast and Furious 6.

10. PITBULL ($11 MILLION)
Mr. Worldwide ameingiza kiasi hiki cha pesa kikubwa kutokana na album yake ya Global Warming na pia uwakilishi wake katika kampuni ya kodak na Dr. Pepper.

11. DRAKE ($10.5 MILLION)
Pamoja na kutokutoa album mpya yoyote kwa mwaka jana, Drake kapata pesa kwa matamasha na filamu kidogo alizoigiza.

12. SNOOP LION ($10 MILLION)
Muonekano wa snoop baada ya kubadili jina kwenda kua Snoop Lion kumemuweka msanii huyu katika hatua nzuri kwa mashabiki wa rege na  muonekano wake kuwekwa kwenye catalog kibao na kumuingizia pesa mtaalam huyu wa hiphop.

13. EMINEM ($10 MILLION)
Marshall kaweza kuingiza pesa nyingi baada ya kuuza sana album zake. Eminem sio mzuri sana wa biashara na wala hakufanya show nyingi kwenye kipindi hiki ila jamaa anauza sana album zake za sasa na pia za zamani.

14. KENDRICK LAMAR ($9 MILLION)
Kendrick ambae ni ingizo jipya kutoka kwa Dr. Dre mwaka jana alifanya zaidi ya shows 100. Hii imemueka katika list ya watu walioingiza pesa nzuri mwaka 2013.



clouds stream