Tuesday 18 March 2014

DAVID MOYES ASEMA KIBARUA CHAKE BADO KIKO SALAMA NA HAKITAOTA NYASI MAPEMA.



Akiongea kabla ya mechi dhidi ya Olympiakos, David Moyes amesema kua kazi yake kama kocha wa Manchester United bado iko salama kwa kipindi hiki. Man united wanatarajia kucheza na timu ya Ugiriki katika ligi ya mabingwa mzunguko wa 16 ikiwa chini kwa mabao 2-0.
Kwa maneno yake Moyes mwenyewe alisema kua ana imani kubwa kua klabu ya Man United itazidi kuwa nae kwa kipindi cha mkataba wake wa miaka 6. Akaongezea kwa kusema kua klabu hio haina mazoea ya kuangalia mipango ya muda mfupi bali wanatizamia mipango ya muda mrefu.
Pia Moyes amesema kua anapewa faraja kubwa ndani ya uongozi wa Man United ikiwemo support kubwa kutoka kwa David Gill, Sir Alex na pia bodi. Pamoja na uhakika wa kazi yake, David amekiri kua kazi ndani ya Man United sio rahisi kama alivyotarajia.

KUTOKA: CNN.COM

clouds stream