Monday 3 March 2014

MOVIE ZINAZOTARAJIWA KUFANYA POA 2014


X-MEN: DAYS OF THE FUTURE PAST (ITATOKA 5/23/2014)
Movie hii imechezwa na waigizaji maarufu kama ian mckellen, patrick stewart, jennifer lawrence, james mcavoy,halle berry, michael fassbender, and hugh jackman. Story iliyobeba movie hii ni juu matukio ambayo yanaleta ulimwengu wa sasa na wa baadae kukutana katika nyakati moja ambapo kisayansi inaleta mkanganyiko mkubwa ambao unaitaji watu wenye nguvu zisio za kawaida kutumika ili kutetea dunia isipotee. katika hali ya kawaida pia, movie hii inaelezea kuwindwa kwa watu wenye nguvu zisizo za kawaida (mutants) na hali halisi ya maisha yao. Ni movie inayotarajiwa kuwa na action na effects za kufa mtu.

NOAH: (ITATOKA 3/28/2014)

Movie hii ya Nuhu ni movie ambayo inasimulia habari kama ilivyooandikwa kwenye Bibilia juu ya Nuhu na matendo ya kipindi chake. Movie hii imebeba story tokea Noah ilipopata maono na mpaka kujenga safina ili aweke viumbe vya Mungu kwaajili ya ujio wa mafuriko makubwa yatakayo angamiza kote. Filamu hii imeigizwa na mastaa walioshinda tuzo za ACADEMY kama Russell Crowe, Emma Watson, Logan Lerman na Jeniffer Connelly.

THE AMAZING SPIDERMAN 2:


Muendelezo wa the amazing spiderman ndio huu hapa. Kijana mdogo kwa jina la Peter Parker anaendelea kuulinda mji wa New York dhidi ya ualifu huku pia akijaribu kutuliza akili yake ili aweze kuishi maisha yake kama kijana wa kawaida pia. Safari hii waigizaji kama Gwen Stacy na Jamie Foxx wameongezeka na pia kuonesha kipaji kikubwa cha uigizaji.

300 THE RISE OF EMPIRE
Kama unakumbukumbu nzuri utakua unakumbuka filamu ya 300 spartans ambapo ilizungumzia utawala wa Persia na kijiji kimoja cha Spata ambacho kiligoma kusaliti amri na kujikaza kupambana na jeshi kubwa la Persia. Katika hii mpya, bado mapambano yanaendelea dhidi ya Jeshi hilo wakati pia kunatokea mabadiliko ya kitekinologia na kuchepuka kwa Ugiriki. Sio movie ya kukosa.






GODZILLA:


Jitu la kutisha linalotaka kuharibu dunia kwa asilimia 100 latokea tena. Filamu hii ya Godzilla ni marudio ya Godzilla ya kwanza ambayo bilitoka mnamo mwaka 2004 na kubeba mashabiki kibao wa movie na wenye kupenda hadithi za kutisha. Mwanasayansi kichaa ambae alichanganya mambo nakujikuta akitengeneza li jitu la kutisha kwa jina la Godzilla ambalo linaharibu mali na kuua watu kama sehemu ya starehe yake. Ni noma!



FOR ANY CINEMA STORE THAT WISHES TO POSTS ITS MOVIE CALENDARS, DON’T HESITATE TO CONTACT US




clouds stream