Friday 14 March 2014

SHOWROOM: MUONEKANO WA TOYOTA IST LA MWAKA 2014.

Toyota ist ni moja wapo kati ya magari mengi ya Toyota ambayo yametokea kupendwa na kununuliwa sana katika kipindi cha kuanzia 2013. Pengine ni uwezo wa gari hili kutumia mafuta kidogo au labda muonekano wake uliofanya lipendwe zaidi na watanzania wengi.
kama ni muonekano basi toleo la mwaka 2014 litakufanya upate mshawasha wa kutosha kutamani japo kuliendesha kwa lisaa limoja ama pengine milele.
Toleo la mwaka 2014 pia linaonesha kua halitakua na ulaji mkubwa wa mafuta ambapo lina ukubwa wa injini 1500cc. Bei yake ya awali ni kama Dola za kimarekani 21200 kuelekea 24200.

Angalia muonekano wake:

KWA MBELE
MBELE UPANDE WA PILI
NYUMA
MPANGILIO WA SITI
DASHBOARD
RANGI ZILIZOPO

clouds stream