Monday 24 March 2014

KUA MODEL SIO LAZMA UWE MWEMBAMBA. ANGALIA BIG IS BEAUTIFUL FASHION SHOW YA AUSTRALIA ILIVYOFANA NA MODELS WANENE.

Kuna fikra imejijenga kwa muda mrefu kua ili kua mwanamitindo au kutumika katika maonesho ya mavazi ni lazma uwe mwembamba. Fikra hii imewekwa chini kidogo baada ya wana wanamitindo wa Australia kama Myer, Leona Edminson,Basque Women, Estelle, Maggie T na Lucabella kuweka onesho la mavazi la watu wenye maumbile makubwa. Jambo hili limepongezwa na wadau wa mitindo hasa ukizingatia kua upande wa mavazi kwa watu wenye maumbile makubwa ni kama umesahaulika. Japokua pia kumekua na watu waliopinga na kuliponda tamasha hili wakidai kua itawalemaza watu wenye maumbile makubwa wasijaribu kupungua, watu wengi wamelipokea jambo hilo kwa shangwe wakisema kua watu wote hatuwezi kufanana. Angalia mwenyewe ilivyokua na kama imekuvutia au laa.

















clouds stream