Monday 3 March 2014

HOTELS: CHUMBA CHA MILIONI 104 NA ZAIDI. HOTELI ZA KIFAHARI ZAIDI DUNIANI


Royal Penthouse Suite, Hotel President Wilson, Geneva (TSH mil 104 kwa usiku)
kwa sababu za kiulinzi zaidi pamoja na usalama hakuna hoteli duniani inayosifika kama President Wilson hotel ambapo katika muonekano wa chumba utaona ziwa Geneva na pia ziwa Mont Blanc. Vioo vya chumba hiki vinauwezo wa kuzuia risasi na ina lifti yake binafsi kwa anetumia chumba hicho. Chumba hiki pia kina eneo la mazoezi, chumba cha kikao na pia eneo la muziki.

The Presidential Suite, The Raj Palace Hotel, Jaipur, India (TSH MIL 72 Kwa usiku)






Hoteli ya Raj ina historia ya kua chumba kikubwa zaidi kuliko vyote vyenye hadi ya kiraisi kwa bara Asia. Ukubwa wake ni kama mita mraba 1500. Chumba hiki kimepambwa kwa dhahabu, pembe za ndovu na vioo vilivyowekwa kwa ustadi wa aina yake. Chumba hiki kina bwawa la kuogelea, makumbusho binafsi na uzuri wake unaeza kukufanya usitamani kuondoka.
Ty Warner Penthouse Suite, Four Seasons Hotel, New York (TSH MIL 66.93 kwa usiku)
Chumba hiki kina mita za mraba 400 ambacho kiko juu kabisa na kinakupa muonekano wote wa Manhattan New York.  Chumba hiki kimepambwa na platinum pamoja na dhahabu na kina garden ya ndani kwa ndani. Ukiwa kwenye chumba hiki utapata waiter wako binafsi, mkufunzi wa mazoezi au mesaji wako binafsi pamoja na dereva wako binafsi


Ritz-Carlton Suite, Ritz-Carlton, Moscow (TSH MIL 28.8 kwa usiku)
Dari la hoteli hi kwa kipekee zaidi limefanana nan a tiles safi zenye taa nyingi za rangi mbali mbali kuweka nakshi. Chumba hiki kina mita za mraba 232 na kna eneo la chakula, ofisi, library na kwa sababu ya baridi mjini Moscow sakafu yake ina heater.









clouds stream