Monday 3 March 2014

BURUDANI: UNAWAFAHAMU MAGOLI KIPA TANO BORA WA KIMATAIFA WENYE MAGOLI MENGI KULIKO WOTE DUNIANI? HAWA HAPA.


1.     ROGERIO CENI



ROGERIO CENI ni goalkeeper mwenye uraia wa Brazil ambae anaongoza kwa idadi ya ufungaji wa magoli kwa magoli kipa. Mpaka sasa Rogerio ana jumla ya magoli 112 ambayo 59 kafunga kwa mpira wa adhabu na 53 kafunga kwa njia ya penati



2. JOSE LUIS CHILAVERT



CHILAVERT ni goalkeeper mzaliwa wa Paraguay na umri wake kisoka ni tokea kipindi cha mwaka 1982 mpaka 2004. Chilavert ana magoli 62 na ni kipa pekee mwenye recodi ya kufunga hatrick katika match. Alichezea timu kama Real Zaragoza, velez, sarsfield, penarol, stasbourg, sportive luqueno na guarani.

3. DIMITAR IVANKOV

DIMITAR ni mchezaji kutoka Bulgaria na amecheza mpira tokea mwaka 1996-2011. Katika kipindi chake, alifunga magoli 42 kwa njia ya penati. Ni kipa ambae alikua anaaminika sana kuhusu swala la kupiga penat. Alichezea timu kama levski sofia, kayserispor na bursaspor.

4. RENE HIGUITA

Golikipa huyu wa Colombia ni kipa aliyejaa sifa na madoido kibao akiwa golini. Ni golikipa aliye wai kuokoa mpira kwa kuruka kama scorpion. Kipa huyu amekaa golini kwanzia mwaka 1985-2010. Alistaafu mpira akiwa na magoli 41. Alifanikiwa kuchezea timu kama depotivo rionegro, guaros, independiente na real vallaroidoid

 



5. JOHNNY VEGAS FERNANDEZ




 
JOHNNY VEGAS ana jumla ya magoli 39 na ni mzaliwa wa Peru. Kipa huyu alianza kucheza mpira wa kulipwa kwanzia 1997 ambapo hadi sasa yupo golini akichezea cienciano.










clouds stream