Tuesday 4 March 2014

lupita nyong'o kunyakua tuzo za Oscars

Kama mwaka mmoja tokea sasa ningekuuliza Lupita Nyong’o ni nani nadhani usingekua hata na wazo moja juu yake. Lupita ni muigizaji mwenye asili ya Kenya aliyezaliwa Mexico mwaka 1983 mwezi wa 3 tarehe 1. Anafahamika zaidi kutokana na filamu yake ya kwanza kuigiza kama muigizaji msaidizi iitwayo 12 years a slave (miaka 12 mtumwa).


Nyota ya muigizaji huyu imekua sana pale ambapo alifanikiwa kuchukua tuzo ya muigizaji bora msaidizi wa kike katika tuzo za Oscars huko marekani. Katika filamu hio ya 12 years a slave, Lupita liigiza kama binti mtumwa aitwae Patsey ambae pamoja na kua mtumwa alichukiwa sana na mke wa mmiliki wakeAkiwa katika tuzo za Oscars, Lupita alipendeza sana na vazi lake lenye rangi iliyopata umaarufu iitwayo kwa sasa “Nairobi Blue”






clouds stream