Wednesday 22 February 2017

Maalim Seif ‘Amganda’ Dk.Shein Angoke Madarakani

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad.
img-20161130-wa0008

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, amemshauri Rais Dk. Ali Mohammed Shein kuachia madaraka kabla ya kuondolewa kwa nguvu na jumuiya za kimataifa kwa kile alichodai alimshinda katika uchaguzi Mkuu Oktoba, mwaka 2015.

Maalim Seif alisema hayo wakati katika ziara yake ya wiki mbili kisiwani Pemba ya kujenga chama, kwenye ukumbi wa Dolfin Bopwe, ambapo Maalim Seif alimtaka Rais Shein kuachia madaraka kutokana na kushindwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

”Kama hakubali kuondoka kwa hiari yake basi amuangalie mwenzake Yahya Jammehy wa Gambia alivyoondoka madarakani bila ya hiari yake,” .

Amesisitiza kuwa ana uhakika na ushahidi uliowazi kuwa alimshinda Dk.Shein, lakini alitumia nguvu ya majeshi na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kufuta uchaguzi, jambo ambalo halimo katika taratibu.

Katika hatua nyingine Maalim Seif amewataka wanachama wake kutokubali kufanywa Chombo cha machafuko hivyo aliwasihi wanachama wake utulivu kwani muda wa kukabidhiwa madaraka umefika.

Hadi sasa katika ziara yake Maalim Seif ameshafungua matawi 12 ya chama hicho kwa Mkoa wa kusini Pemba na sasa anaelekea Mkoa wa Kaskazini.

clouds stream