Thursday 9 February 2017

Trump Agonga Mwamba Mahakama Ya Rufaa, Aazimia Kupambana Na Mihadarati


Rais wa Marekani Donald Trump trump.
Rais wa Marekani Donald Trump trump.

img-20161130-wa0008

Mahakama ya Rufaa nchini Marekani imekataa kuirudisha tena marufuku iliyowekwa na Rais wa nchi hiyo, Donald Trump kwa wasafiri kutoka nchi saba za Kiislamu na Wakimbizi wote kuingia nchini humo.

Jopo la Majaji watatu kwa kauli moja limekataa kuupindua uamuzi uliotolewa na Jaji kutoka Mji wa Seattle, ambaye wiki iliyopita alizuia sehemu za amri iliyotolewa na Rais huyo wa Marekani.

Habari zinasema kwamba uamuzi huo kwa sasa utapelekwa katika Mahakama ya Juu zaidi.

Na muda mfupi tu baada ya uamuzi huo wa mahakama kutangazwa, Rais Donald Trump aliwaambia waandishi wa habari kwamba ana uhakika mwisho wake ataibuka mshindi.

 ”Ni uamuzi wa kisiasa na tutaenda kukutana mahakamani. Natarajia kufanya hivyo, tuna hali ambayo usalama wa nchi yetu uko hatarini na ni hali mbaya sana,” amesema Trump.

Katika hatua nyingine tena Rais Trump ametangaza mfululizo wa amri za Rais kwa lengo la kupunguza uhalifu.

Akizungumza wakati wa kuapishwa kwa Mwanasheria Mkuu wa nchi hiyo, Trump amesema uhalifu umeongezeka nchini Marekani na utawala wake utalishughulikia suala hilo kuanzia sasa.

Amri hizo zilizotangazwa ni pamoja na kukabiliana na magenge ya madawa ya kulevya na wafanyabiashara za kihalifu.

clouds stream