Monday 6 February 2017

Wadudu waharibifu wavamia mimea Afrika

Kiwavi hao kwa jina armyworm wanavamia mimea kama wanajeshi

Kiwavi hao kwa jina armyworm wanavamia mimea kama wanajeshi
img-20161130-wa0008

Wanasayansi wanataka hatua za dharura kuchukuliwa ili kuzuia kuenea kwa wadudu wanaoharibu mimea barani Afrika Afrika.

Kituo cha kimataifa cha kilimo cha sayansi ya baiolojia {Cabi} kimesema kuwa wadudu hao ni tishio kubwa la usalama kwa chakula pamoja na biashara ya kilimo.

Kiwavi huyo ambaye anatoka Afrika Kaskazini na Kusini aligunduliwa kwa mara ya kwanza barani Afrika mwaka uliopita.

Wataalamu wanasema kuwa mdudu huyo huenda akawasili barani Asia na eneo la Mediteranea katika kipindi cha miaka michache ijayo.

Shirika la chakula na kilimo limepanga mazungumzo ya dharura kuhusu swala hilo.

Kiwavi huyo amepewa jina 'armyworm' kwa sababu anakula mimea iliopo katika njia yake akiendelea kusonga mbele kama mwanajeshi.

Mawanasayansi mkuu wa Cabi Matthew Cock: Mdudu huyu mvamizi sasa amekuwa changomoto kubwa kwa sababu anaenea katika Afrika ya tropiki mbali na kuwa na uwezo wa kusambaa hadi bara Asia.

Hatua za dharura zitahitajika kuzuia uharibifu wa mimea na maisha ya wakulima.

Wanasayansi wanadhani kiwavi hao ama mayai yao huenda yaliwasili barani Afrika kupitia mazao yalioagizwa kutoka nje.

Wakati anapoanza kuishi katika eneo moja ,nondo mkubwa wanaweza kuruka umbali mkubwa na kuenea kwa haraka.

clouds stream