Tuesday 24 October 2017

Buffon achukua nafasi ya Neuer kikosi bora cha Fifa

Gianluigi Buffon


Gianluigi Buffon ameshinda Serie A mara kumi



Shirikisho la soka duniani Fifa limetangaza kikosi bora cha soka ya wanaume duniani mwaka 2017 ambapo kuna mabadiliko matatu kutoka kwa kikosi kilichotangazwa mwaka 2016.

Kwenye kikosi hicho, maarufu kama Fifpro World XI, mlindalango Gianluigi Buffon amechukua nafasi ya Manuel Neuer, naye beki wa AC Milan Leonardo Bonucci akachukua nafasi ya kigogo wa Barcelona Gerard Pique kwenye safu ya ulinzi.

Mshambuliaji wa PSG Neymar, ambaye ndiye mchezaji ghali zaidi duniani naye ameingia nafasi ya Luis Suarez katika safu ya mashambulizi.

Kikosi hicho kina wachezaji watano kutoka Real Madrid, wawili wa Barcelona, wawili wa PSG, mmoja wa Juventus na mmoja kutoka AC Milan.

Hakuna mchezaji hata mmoja wa Ligi ya Premia aliyefanikiwa kujumuishwa katika kikosi hicho.

Fifpro World XI

Mkufunzi bora duniani soka ya wanaume

Zinedine Zidane amemshinda meneja wa Chelsea Antonio Conte baada ya kuongoza Real Madrid kushinda La Liga msimu uliopita kwa mara ya kwanza tangu 2012 na kushinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mtawalia msimu uliopita.

Conte alishinda Ligi ya Premia msimu uliopita.
Massimiliano Allegri wa Juventus, ambaye aliongoza klabu yake kushinda Serie A na Coppa Italia msimu uliopita alikuwa wa tatu.

Mkufunzi bora soka ya wanaume
Zinedine Zidane - 46.22%Antonio Conte - 11.62%Massimiliano Allegri - 8.78%

Mkufunzi bora duniani soka ya wanawake

Kocha wa Uholanzi Wiegman aliyeongoza Uholanzi kushinda Euro 2017 nyumbani kwao amechukua taji hilo.Waliwalaza Denmark kwenye fainali.

Sarina Wiegman akipokea taji lake
Sarina Wiegman akipokea taji lake

Mkufunzi bora wa soka ya wanawake
Sarina Wiegman - 36.24%Nils Nielsen - 12.64%Gerard Precheur - 9.37%
   

Kipa bora zaidi

Mshindi wa Kombe la Dunia na mshindi wa Serie A mara 10 Gianluigi Buffon ndiye mshindi wa tuzo ya mlindalango bora duniani mwaka huu.

Aliwasaidia Juventus kushinda taji la ligi mara ya sita mtawalia msimu uliopita.
Aidha, alicheza dakika 600 Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya bila kufungwa.

Buffon, 39, amewashinda kipa Keylor Navas, wa Real Madrid na Manuel Neuer wa Bayern Munich.
"Ni heshima kubwa sana kwangu kupokea tuzo hii katika umri wangu huu," alisema Buffon.

Uchezaji haki

Mchezaji wa Togo Francis Kone, ambaye alimfanyia huduma ya dharura kipa wa Bohemians 1905 Martin Berkovec uwanjani wakati wa mechi ya ligi Jamhuri ya Czech mwezi Februari ametunukiwa tuzo ya uchezaji wa haki.

clouds stream