Monday 23 October 2017

WAZIRI WA MAGUFULI ATANGAZA BOMOABOMOA KUBWA NCHI NZIMA




Bomoa bomoa kufanyika nchi nzima.



Hatimaye baada ya Bomoa bomoa kutikisa Mbezi ya Kimara,Serikali imewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri, Maafisa Ardhi, Maafisa Ujenzi na Maafisa Mipangomiji kuweka alama za X na kuvunja majengo yote yanayojengwa katika miji yao bila kibali na yale yanayojengwa katika viwanja vya watu wengine walio na hati.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi alipofanya ziara wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa alpoenda kutatua mgogoro wa ardhi.
Waziri Lukuvi amesema tatizo la ujenzi holela linaanza pale ambapo Wakurugenzi wa Halmashauri, Maafisa Ardhi, Maafisa Ujenzina Maafisa Mipangomiji wanaacha majengo yanaibuka katika miji yao bila kujua ujenzi huo una kibali au unajengwa katika kiwanja chenye hati na muhusika wa hati hiyo ndio anayejenga.

“Hatuwezi kuendelea na zoezi la kufanya urasimishaji wa makazi kila siku wakati chanzo cha tatizo hilo kinajulikana, kwa hiyonaagiza Wakurugenzi, Maafisa Ardhi, Maafisa Ujenzi na Maafisa Mipangomiji kuweka x katika majengo yote yanayojengwa bilavibali na ujenzi unaofanywa kwenye viwanja vya watu masikini kwa dhuruma” amesema Lukuvi.

Watu watakaokumbwa na bomoa bomoa hiyo ni wale waliojenga bila vibali, kujenga katika maeneo yasiyoruhusiwa pamoja nawaliojenga baada ya kuvamia maeneo.

clouds stream