Monday 2 October 2017

Mshambuliaji Stephen Paddock aua watu 50 Las Vegas, Marekani

People fleeing from scene of country music festivalZaidi ya watu 50 wauawa kwa wapigwa risasi Las Vegas Marekani



Zaidi ya watu 50 wameuawa na takriban 200 kujeruhiwa kwenye ufyatuaji wa risasi wakati wa tamasha la muziki huko Las Vegas, Marekani.
Mtu mwenye bunduki mwenye umri wa maiak 64 Stephen Paddock alifyatua risasi kutoka ghorofa ya 32 kwenye hoteli ya Mandalay Bay, kwenda kwa tamasha lililokuwa likiendelea nje.
Eneo la mauajiEneo la mauaji

Polisi wanasema mshukiwa ambaye alitajwa kuwa mkaazi wa mji huo na ambaye hakutajwa jina ameuawa.

Mamia ya watu walikimbia eneo hilo na milio ya risasi ikasikika kwa muda kwenye video zilizochapishwa katika mitandao ya kijamii.

Ufyatuaji huo ulitokea mwendo wa saa 05:30 GMT na walioshuhudia walisema kuwa mamia ya risasi zilifyatuliwa.

Usafiri wa ndege ulisitishwa kutoka uwanja wa ndege wa McCarran mjini Las Vegas

People fleeing from scene of shootingZaidi ya watu 50 wauawa kwa wapigwa risasi Las Vegas Marekani

Police are seen crouching in front of vehicle outside hotelPolisi wakiwa nje ya hoteli ya Mandalay

clouds stream