Sunday 8 October 2017

Serikali Yabadili Mfumo Wa Ulipaji Mishahara Kwa Watumishi Kubana Matumizi



Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango.


Serikali imesema kuwa itaanza kutumia mfumo wa kielektroniki katika kulipa mishahara badala ya matumizi ya karatasi za kutolea nakala za malipo ya mshahara ‘salary slip’ kwa watumishi wa umma.
Lengo la hatua hiyo imetajwa kuwa ni kupunguza gharama za uendeshaji.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Fedha na Mipango, imesema watumishi wa umma wataanza kutumia mfumo wa kieletroniki katika masuala yote ya kiutendaji, ikiwemo kukamilisha mahitaji ya taasisi za fedha watakapokuwa wakihitaji mkopo au wanaposhughulikia mafao kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii.

Taarifa hiyo imesema hata wastaafu watapaswa kufuata utaratibu huo mpya pamoja na wadau wengine wanaoshirikiana nawafanyakazi wa umma yakiwemo mashirika ya bima.

Kila mtumishi au mstaafu serikalini atahitaji kujisajili ili kupata nakala hiyo kulingana na utaratibu wa kujisajili na kutumia mfumo utakaotolewa na waajiri.

“Kutokana na gharama kubwa za uchapishaji, usambazaji na usumbufu wa kuzitafuta nakala hizo, wizara imeandaa mfumo wa kielektroniki wa utoaji wa hati za malipo ya mshahara ujulikanao kama ‘government salary slip self service’,” imesema sehemu ya taarifa hiyo

clouds stream