Wednesday 11 October 2017

Watatu Wengine Wafa maji Ziwa Victoria


Related image


Watu watatu wamekufa maji ndani ya Ziwa Victoria katika Kisiwa cha Ilamba wilayani Muleba baada ya mtumbwi waliokuwa
wakisafiria kuzama.

Watu hao walikuwa wakitoka kuchota maji Kisiwa cha Mazinga na mtumbwi wao kuzama baada ya kupigwa upepo mkali na
kupinduka.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustino Olomi amesema watu hadi jana walifanikiwa kuopoa mwili mmoja.

Amesema miili ambayo haijapatikana ni ya Superius Severine (27) Mkazi wa Kijiji cha Nyakitaba na Evelius Zephrine (22) waMubunda Kitoko Wilayani Muleba Kamanda Olomi amesema mwili uliopatikana ni wa Adela Andrea (26), Mkazi wa Kijiji cha Itongo.

Amesema Nelson Boniphace (20), mkazi wa Kisiwa cha Ilamba aliogelea na kuokolewa.
Mtumbwi huo uliokuwa na madumu 33 ya maji amesema unamilikiwa na Rashidi Sabini (33), mkazi wa Kijiji cha Ilamba.

Tukio hili linatokea wakati ambapo Watanzania wakiomboleza vifo vya watu 12 walifariki katika Ziwa Victoria baada ya gari ndogo daladala aina ya Hiace waliokuwa wakisafiria kupata ajali na kuzama katika Ziwa Victoria.

clouds stream