Sunday 1 October 2017

Professor Jay Afunguka Machungu Ya Kubomolewa Nyumba





Mbunge wa Mikumi (Chadea), Joseph Haule ‘Professor Jay’ ametumia mitandao yake ya kijamii kueleza machache na uchungu
aliousikia kuhusiana na kubomolewa kwa nyumba za wananchi huko Mbezi Kimara ikiwemo nyumba yake.
Professor Jay ameandika yafuatayo;
“Mimi ni mmoja wa wahanga wa hili zoezi la kubomolewa nyumba zetu huku Mbezi Kimara Tarehe 29/9/ 2017. Jana (juzi) nikiwa
katika majukumu jimboni Mikumi Majira ya saa kumi mbili hivi jioni, nilitaarifiwa kwamba, watu wa Tanroads wakiwa
wameambatana na grader mbili na magari mawili ya polisi (defenders) yenye askari waliokuwa na silaha mbalimbali za moto
walikuwa wanabomoa nyumba yangu, sijawahi kuumia kiasi hiki.
“Nimesikitishwa sana jinsi Tanroads wanavyoweza kujichukulia maamuzi bila ya kujali mhimili muhimu wa Mahakama wametoa
maagizo gani. Na taratibu zilizotumiwa kubomoa nyumba yangu bila ya mimi na Tanesco kupewa taarifa saa kumi na mbili jioni
(haukuwa muda wa kazi). Poa kubomoa nyumba huku Umeme ukiwa unawaka ni kitendo ambacho kwanza kina hatarisha maisha
ya wabomoaji wenyewe, maisha ya familia yangu pamoja na majirani zangu, LIMENISIKITISHA zaidi.
Nasema hivi kwasababu Tanesco wamenipigia simu baada ya masaa 24 au zaidi baada ya zoezi la kubomoa nyumba kufanyika
kunitaarifu kuja kukata Umeme kabla ya ubomoaji huo, pindi nilipo waambia kwamba mbona nyumba IMESHABOMOLEWA kabisa
na sijaweza kuokoa kitu chochote na hata hiyo meter yenu mnayoiulizia mkaitafute kwenye kile kifusi cha nyumba yangu
kilichokusanywa kwa pamoja na watu wa Tanroads. Tanesco walishangazwa sana kuvunjwa nyumba yangu kwa taratibu hizo.

Lakini naamini kila kitu kinatokea kwa sababu maalum. Nimejifunza kumtegemea Na kumshukuru Mungu kwa kila jambo. Na hili
ni moja ya mitihani ya hapa duniani. Nimepokea na kumsikiliza Mungu ana mipango gani juu yetu katika familia yangu mbeleni.
Tumelipokea na Naamini tutashinda.”

clouds stream