Tuesday 24 May 2016

Magufuli Ateua Mwanasheria, Mshauri Wa Uchumi


Magufuli Ateua Mwanasheria, Mshauri Wa Uchumi


Tarehe May 24, 2016Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Gerson J. Mdemu kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Kabla ya Uteuzi huo, Bw. Gerson J. Mdemu alikuwa Karani wa Baraza la Mawaziri (Cabinet Clerk).
Bw. Mdemu anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Tulia Ackson ambaye amechuguliwa kuwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Profesa Longinus Rutasitara kuwa Mshauri wa Rais, masuala ya uchumi.
Kabla ya uteuzi huo Profesa Longinus Rutasitara alikuwa Mhadhiri wa Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi  imeeleza kuwa uteuzi huu unaanza mara moja.

clouds stream