Friday 13 May 2016

Sakata La ‘Baby’ Bungeni, Wabunge 53 Ukawa Wajitoa TWPG

Sakata La ‘Baby’ Bungeni, Wabunge 53 Ukawa Wajitoa TWPG

Tarehe May 13, 2016Mbunge wa Kawe Halima Mdee.
Mbunge wa Kawe Halima Mdee.
Mbunge wa Kawe Halima Mdee.
Hatimaye Wabunge wanawake 53 wa kambi ya upinzani kutoka vyama vya CUF na Chadema wamejitoa kwenye Umoja wa Wabunge Wanawake (TWPG) kwa madai ya kudhalilishwa na Mbunge wa  Ulanga, Godluck Mlinga (CCM.
Akichangia hoja Bungeni hapo mei 5 mwaka huu Mlinga alisema wabunge hao kutoka Chadema walipata ubunge kwa njia ya mapenzi baada ya kuwa ‘baby’ wa watu.
“Kila mwanamke ndani ya chadema kaingia ubunge kwa sifa yake lakini sifa kubwa ni lazima uwe baby (mpenzi) wa mtu. Ndani ya Chadema kuna wapenzi wa jinsia moja,” alisema Mlinga.
Katika barua yao ya kujitoa jana iliyosainiwa na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee kwa niaba ya wabunge wenzake wa kambi ya upinzani na nakala kupewa Spika, Job Ndugai, ilieleza kuwa kauli ya Mlinga inadhalilisha wabunge hao, utu na heshima ya mwanamke.
“Licha ya juhudi zilizofanywa na wabunge wa upinzani za kutaka mbunge husika(Mlinga) afute kauli yake , juhudi hizo hazikuzaa matunda kutokana na Naibu Spika(Tulia Ackson) kupuuza miongozo iliyokuwa ikiombwa.
“Na kikubwa alichokifanya baada ya mbunge (Mlinga) kumaliza kutukana ni kuwataka watu wa hansard wafute kwenye kumbukumbu za Bunge, kitu ambacho ni kinyume na matakwa ya Kanuni za Bunge,”alisema Mdee kwenye barua hiyo iliyosainiwa na wabunge wa CUF 10 na wa Chadema 43.
Alisema wabunge wa upinzani walisononeshwa zaidi na wabunge wenzao wanawake wa CCM, wakiongozwa na aliyekuwa Katibu wa TWPG, Angela Kairuki na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge,Vijana, Ulemavu na Ajira, Jenista Mhagama kushangilia udhalilishaji huo.

clouds stream