Thursday 26 May 2016

Mrema ‘Amvaa’ Maalim Seif

Mrema ‘Amvaa’ Maalim Seif

 

V 3Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Augustino Mrema.

Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Augustino Mrema,  amelaani hatua ya Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif kutangaza kumwondoa Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein  madarakani kabla ya 2020 huku akiwataka wazanzibar kutoyumbishwa na kauli za mwanasiasa huyo.

Amesema  amani ya Zanzibar ni muhimu kuliko maslahi binafsi hivyo ni vyema kuzitafakari kauli ambazo zinaweza kuleta machafuko na kudai kuwa hakuna mtu aliye juu  ya sheria hivyo kuwepo kwa watu wanaochochea  vurugu  ni kama waahini na kwamba ni vyema hatua zichukuliwe dhidi yao katika kuhakikisha  wananchi wanakuwa salama.

Mrema amesema kwamba amani ya Zanzibar ikiharibika hata bara haiwezi kuwa salama hivyo ni vyema kauli za kuvuruga amani zizingatiwe ili kulinda maslahi ya wananchi wa pande zote mbili.

“Zanzibar ina historia ya kuuawa watu mwaka 2001,kutokana na vurugu za kisiasa hivyo lazma kwa sasa jambo lolote la kiuchochezi liangaliwe kwa macho mawili dhidi ya watu wanaotaka kuvuruga amani katika mazingira hayo,” ameonya.

Amesisitiza  kuwa hakuna chama cha siasa ambacho kinajengwa kwa kususia uchaguzi bali kufanya hivyo ni kuwanyima wapiga kura haki pia ni hatari na kunaweza kusababisha chama kusambaratika kama kulivyotokea kwa baadhi ya vyama mfano, UPC cha Uganda na vinginevyo.

Pamoja na hayo mrema amefafanua kwamba mahakama ya ICC haingalii tu viongozi wa serikali bali hata viongozi wa kisiasa ambao wamesababisha mauaji kutokana na kauli wanazozitoa na kuwataka wahisani kutoingilia mambo ya ndani ya nchi kwani kusitisha misaada kwa hoja ya kufutwa uchaguzi wa Zanzibar na sheria ya mitandao ni kuingilia uhuru wa watanzania.

clouds stream