Thursday 26 May 2016

Vifaranga 5,000 Vyakamatwa Uwanja Wa Ndege


Vifaranga 5,000 Vyakamatwa Uwanja Wa Ndege


Tarehe May 26, 2016airport
Serikali inashikilia jumla ya vifaranga 5,000 vya kuku baada ya kuvikamata vikiingizwa nchini kutokea nchini Malawi kwa kutumia vibali visivyo halali.
Akizungumza na wanahabari katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, ,Maria Mashingo amesema kibali kilichotumika kuingiza vifaranga hivyo vyenye thamani ya milioni 20 ni batili kwani kilitolewa mwaka 2014 kwa mfanyabiashara ambaye aliingiza kuku mama ambao huruhusiwa kisheria.
“Hakuna ruhusa ya kuingiza vifaranga kwani huwa na magonjwa ambayo yanaweza kuambukiza kwa kuku wanaozalishwa hapa kwetu!,” alisema Mashingo.
Mashingo aliongeza kuwa, mbali na magonjwa, endapo vifaranga hao wangefanikiwa kupitishwa katika uwanja huo wangeweza kuua soko la wafanyabiashara wa ndani.
Mwaka 2010 serikali ilipiga marufuku kuingizwa kwa vifaranga nchini ili kuiepusha nchi na ugonjwa wa mafua ya ndege ambao umekuwa ukiripotiwa kulipuka katika nchi mbalimbali.

clouds stream