Friday 13 May 2016

Rais Wa Brazil Dilma Rousseff Atumbuliwa

Rais Wa Brazil Dilma Rousseff Atumbuliwa

Tarehe May 12, 2016Rais Dilma Rousseff.
Rais Dilma Rousseff.
Rais Dilma Rousseff.
Hatimaye, Bunge la Seneti Brazil limepiga kura kuamua kuidhinisha kura ya kutokuwa na imani dhidi ya kiongozi wa taifa hilo Dilma Rousseff.
Kutokana na kura hiyo Rais Dilma  atasimamishwa kazi ya urais kwa siku zisizozidi 180 wakati bunge hilo la Seneti litakagua tuhuma zinazomkabili.
Bi Rousseff anatuhumiwa kubadili kinyume cha sheria fedha za serikali kuficha nakisi inayoongezeka ya umma kufuatia kuchaguliwa kwake tena mnamo 2014, tuhuma  ambazo amezikana.
Maseneta 55 waliunga kuidhinishwa kura hiyo ya kutokuwab na imani dhidi ya 22 bungeni katika kikao cha zaidi ya saa 20.
Kufuatia kusimamishwa kwa Rais huyo  Makamu wa rais Michel Temer  atashikilia madaraka wakati kesi dhidi ya Bi Rousseff inaendelea.

clouds stream