Wednesday 11 May 2016

Neema Ya Gesi Yazidi Kunukia

Neema Ya Gesi Yazidi Kunukia

Tarehe May 11, 2016picha saba
picha saba
Baadhi ya mitambo ya kuchakata gesi katika kituo cha Madimba mkoani Mtwara
Ujenzi wa Mradi wa Kusindika Gesi (LNG) mkoani Lindi utakaowezesha nchi kuanza kufanya biashara ya gesi nje ya nchi umeanza baada ya jana wadau sita wa mradi huo kukutana na kupeana elimu kabla ya mchakato mzima kuanza wakati wowote mwaka huu.
Akizungumza jana katika mkutano huo, Mkurugenzi wa Utafiti wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Kelvin Komba alisema tayari ardhi imepatikana ya hekta 2,071 kwa ajili ya mradi wa LNG huku hekta nyingine 20,000 zinazozunguka eneo la mradi huo, zikitengwa kwa ajili ya viwanda.
Alifafanua kuwa alisema mkutano huo ni kuanza taratibu za awali za kuwekeza na kuuza gesi kwa kutolewa kitaalamu rasilimali hiyo kwenye visima na kufikishwa katika mtambo huo wa LNG ambao utaigeuza kuwa kimiminika ili ifae kuingizwa katika matangi na kusafirishwa kwa meli kwenda katika masoko mbalimbali duniani.
Mradi huo mkubwa wenye thamani  inayofikia zaidi ya Dola za Marekani bilioni 60, utatoa karibu ajira 20,000 na utawezesha nchi kukua kiuchumi.
Alizitaja kampuni sita zinazoshirikiana katika ujenzi wa mtambo huo ni TPDC, BG Group, Ophir Energy, Statoil, Exxon Mobil na Pavilion Energy. Mradi huo thamani yake ni kuanzia Dola za Marekani bilioni 30 mpaka bilioni 60.

clouds stream