Thursday 26 May 2016

Serikali: Marufuku Kusafirisha Wanyama Hai

Serikali: Marufuku Kusafirisha Wanyama Hai

Tarehe May 26, 20168-1-1
8-1-1
Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe
Serikali imepiga marufuku kusafirisha wanyamahai wote nje ya nchi kwa miaka mitatu kuanzia leo hadi hapo idara ya wanyamapori itakapokuja na utaratibu mpya wa kuwasafirisha.
Hayo yamesemwa bungeni na Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe wakati akifanya majumuisho ya hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya wizara yake kwa mwaka 2016/17.
“Kuanzia sasa  kwa miaka mitatu serikali imepiga marufuku usafirishaji wa wanyamahai wote kwenda nje ya nchi… Hata chawa za Tanzania hataruhusiwa kusafirishwa nje,” alitangaza Waziri Maghembe.
Maghembe alisema wanyama wengi kutoka Tanzania hupelekwa Hong Kong, Thailand, Ulaya Mashariki na kwingineko duniani jambo linalosababisha ukosefu wa mapato kwa serikali kwani wanyama hao huingizia mapato nchi hizo badala ya Tanzania.

clouds stream