Wednesday 11 May 2016

TRA Yaiachilia Sukari Iliyokamatwa Mbagala

TRA Yaiachilia Sukari Iliyokamatwa Mbagala

Tarehe May 11, 2016sukari2
sukari2
Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imeachilia tani 6,757 za sukari iliyokutwa kwenye maghala ya forodha huko Mbagala nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam baada ya kubaini kuwa iliingizwa nchini kihalali.
Mkurugenzi wa Idara ya Elimu na Huduma kwa Mlipakodi wa (TRA) Richard Kayombo ameviambia vyombo vya habari kuwa sukari hiyo iliingizwa nchini na kampuni ya Al-Naeem na ilikuwa ikisubiri vibali kutoka Bodi ya Sukari, Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) pamoja na kukamilisha taratibu za kodi.
Kwa mujibu wa Kayombo, mmiliki wa shehena hiyo ameruhusiwa kuanza kuisambaza sukari hiyo katika mzunguko wake wa kibiashara na kwamba kuwepo kwake sokoni huenda kukasaidia kupunguza bei na makali ya upatikanaji wa sukari nchini.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Kampuni ya Al-Naeem, Eddy Salim amesema baada ya ruhusa hiyo ya serikali, wamejipanga kuhakikisha sukari inasambazwa katika maduka yao yote huku wakihakikisha kuwa bei inabaki kuwa ya kawaida.

clouds stream