Saturday 21 May 2016

Majaliwa Abariki ‘Kutumbuliwa’ Kwa Kitwanga

Majaliwa Abariki ‘Kutumbuliwa’ Kwa Kitwanga

Tarehe May 21, 2016
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema uamuzi wa Rais, Dkt. John Magufuli kutengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga umefuata kanuni za utumishi wa umma ambazo zinakataza kulewa wakati wa kazi.
Majaliwa amesema zipo sheria za utumishi ambapo mtu hutakiwi kunywa pombe na wala hupaswi kulewa ukiwa kazini ili kusudi mtumishi uweze kuwa na akili zako zote timamu zitakazokuwezesha kufanya kazi za Serikali kwa ufanisi.
“Kuna swali aliloulizwa kuhusiana na Wizara yake na kulijibu katika muonekano ulioonyesha kuwa amelewa kiasi cha kupelekea kutojibu swali hilo vizuri na swali hilo litapaswa kurudiwa kuulizwa tena baada ya wabunge kuomba muongozo wa swali hilo,” ameongeza.

clouds stream