Saturday 21 May 2016

Maoni Ya Zitto Kabwe ‘Kutumbuliwa’ Waziri Kitwanga

Maoni Ya Zitto Kabwe ‘Kutumbuliwa’ Waziri Kitwanga

Tarehe May 21, 2016

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe
Mbunge wa Kigoma Mjini na kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe ametumia ukurasa wake wa facebook kuelezea   maoni yake  baada ya Rais Magufuli kufanya maamuzi ya kumfuta kazi Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Charles Kitwanga.
Kwa mujibu wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu, imebainisha kuwa   Waziri huyo ametolewa madarakani  kufuatia  kuingia bungeni jana asubuhi na kujibu swali lililoelekezwa kwa Wizara yake akiwa amelewa.
“Uamuzi wa Rais kumfukuza kazi Waziri wa Mambo ya Ndani unatuma ujumbe mmoja – hataki mchezo. Rais amethibitisha kuwa anao uwezo wa kutumbua hata aliowateua. Ni maamuzi muhimu sana kwa Kiongozi wa aina yake. Wale vijana waliokuwa wanatumwa kumtetea wasimame kumtetea. Rais kaonyesha Uongozi ‘ no nonsense “Alisema Zitto Kabwe

clouds stream