Monday 3 July 2017

China: Hatua ya meli ya Marekani kukaribia kisiwa ni uchokozi mbaya

The USS Stetham, in a photo from 2015, arrives at a port in Shanghai

Meli USS Stetham
IMG-20170426-WA0006

China imetaja hatua ya manowari ya Marekani kupita karibu na kisiwa kinachozozaniwa kusinia mwa bahari ya China kuwa uchokozi mbaya wa kisiasa na kijeshi.

Manowari ya USS Stethem ilipita karibu na kisiwa kinachozozaniwa cha Triton ambacho ni moja ya visiwa vinavyodaiwa na China na nchi zingine,

Uchina ilijibu kwa kutuma meli za kijeshi na ndege kuenda kisiwa hicho.

Kisa hicho kilitokea muda kabla ya viongozi wa nchi hizo mbili kufafanya mazungumzo ya simu.Map

Eneo la kusini mwa China

Marekani mara kwa mara imeionya China dhidi ya hatua yake ya kunyakua visiwa katika maeneo yanayozozaniwea, lakini china inasema inafanya hivyo kuambatana na haki zake.

China inasema kuwa itafanya kila iwezalo kulinda usalama wake.

Pia imeilaumu Marekani kwa kuchochea vurugu eneo hilo kwa kuwa uhusiano kati ya China na majirani wake wa kusini mwa bahari ya China umeboreka.

Kisiwa hicho kidogo pia kinadaiwa na Vietnam na Taiwan. China imekuwa kwenye mzozo wa umiliki wa maeneo ya bahari na majirani zake kadha miaka ya hivi karibuni.

clouds stream