Monday 17 July 2017

KOREA KUSINI YATAKA MAZUNGUMZO YA KIJESHI NA K. KASKAZINI

_96967737_tensions
IMG-20170426-WA0006

Korea Kusini imependekeza kufanyika mazungumzo ya kijeshi na Korea Kaskazini, baada ya majuma kadhaa ya misukosuko iliyosababishwa na hatua ya Korea Kaskazini kufanya majaribio ya makombora.

Ikiwa mazungumzo hayo yatafanyika, yatakuwa ndiyo ya kwanza katika ngazi ya juu tangu mwaka 2015.

Maafisa wa vyeo vya juu wamesema kuwa mazungumzo hayo yatalenga kusitisha vitendo vyote ambavyo huchangia kuwepo kwa misuguano ya kijeshi katika eneo lenye ulinzi mkali kati ya Kusini na Kaskazini.

Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in tangu mwanzo alikuwa ameashiria kuchukua hatua ya kuleta ushirikiano wa karibu na Korea Kaskazini.

Akitoa hotuba hivi majuzi Mjini Berlin, Moon Jae-in alisema kuwa mazungumzo na Korea Kaskazini yanastahili kufanyika na kutaka muafaka kufikiwa.

Lakini hatua ya Korea Kaskazini kuyafanyia majaribio makombora yake likiwemo la hivi karibuni la masafa marefu, yanaenda kinyume na maazimio ya Umoja wa Mataifa.

Naibu Waziri wa Ulinzi nchini Korea Kusini, Suh Choo-suk, aliuambia mkutano wa wanahabari kuwa mazungumzo yatafanyika eneo la Tongilgak, katika jengo la Korea Kaskazini katika eneo lisilo na ulinzi mkali kati ya nchi hizo mbili.

clouds stream