Thursday 27 July 2017

Miili Ya Watu Wenye Vipara Yafukuliwa Msumbiji

_97090268_bald
IMG-20170426-WA0006

Wakazi wanaoshi katika Wilaya ya Kati ya Milange nchini Msumbiji wanasema kuwa miili ya watu watano wenye vipara imefukuliwa katika kipindi cha miezi mitatu kutokana na imani za kishirikina na kuitaka Serikali kuingilia hali hiyo.

Kwa mujibu wa BBC, Kamanda mmoja wa Polisi nchini Msumbiji, Afonso Dias, amedai kuwa watu wanaamini kuwa mtu mwenye kipara una dhahabu na mnamo Mwezi Juni kumekuwa na msururu wa mauaji ya watu wenye vipara.

Naye Mwakilishi wa Taasisi ya Urithi na Usaidizi wa Haki (IPAJ), Antonio Gussi ameahidi kuwasilisha malalamishi yao kwa mamlaka husika lakini pia akawataka watu kutokubali tamaduni hizo zilizopitwa na wakati katika siku za usoni.

clouds stream