Thursday 27 July 2017

Marekani yawawekea vikwazo maafisa wa vyeo vya juu nchini Venezuela

US Treasury Secretary Steve Mnuchin in Washington, DC, on 26 July 2017

Waziri wa fedha wa Marekani Steve Mnuchin alitangaza vikwazo hivyo
IMG-20170426-WA0006

Serikali ya Marekani imewawekea vikwazo maafisa 13 wa vyeo vya juu nchini Venezuela wakati shinikizo zinazidi kuongezeka dhidi ya Rais Nicolas Maduro kabla ya kura inayokumbwa na utata ya bunge jipya la kuandika katika mpya.

Vikwazo hivyo ni vya kutwaliwa mali ya maafisa hao nchini Marekani na kuyazuia makampuni ya Marekani kufanya biashara nao.

Wale waliolengwa ni pamoja na waziri wa mambo ya ndani na mkuu wa majeshi.

Wiki iliyopita, Rais Donald Trump aliapa kuchukua hatua kali za kiuchumi ikiwa Bwana Maduro ataandaa kura hiyo ya maoni siku ya Jumapili.

President of Venezuela, Nicolas Maduro, speaking to supporters in Caracas, Venezuela, on 25 July 2017.
Rais Nicolas Maduro

Hata hivyo bwana Maduro ametaja vikwazo hivyo kuwa vilivyo kinyume na sheria

Vikwazo hivyo pia vinamlenga mkuu wa baraza la uchaguzi Tibisay Lucena, aliyekuwa makamu wa rais Elias Jaua ambaye anaongoza tume zinaoandaa uchaguzi wa Jumapili.

Kujumuishwa kwa maafisa wa vyeo vya juu kutoka kwa kampuni ya serikali ya mafuta PDVSA na ishara kuwa huenda vikwazo hivyo pia vikalenga sekta ya mafuta nchini Venezuela.

Akitangaza vikwazo hivyo waziri wa fedha wa Marekani Steven Mnuchin alisema kuwa Marekani hauweza kupuuza jitihada za utawala wa Maduro za kuhujumu demokrasia, uhuru na sheria.

A demonstrator prepares to throw a tear gas canister during a strike called to protest against Venezuelan President Nicolas Maduro's government in Caracas, Venezuela on 26 July, 2017.
Maandamano Venezuela

clouds stream